Ruka hadi maudhui kuu

Tafuta

Andika neno au swali ili kutafuta makala za msaada.

Jinsi ya kukubali mwaliko wa timu

Kwenye makala hii

Kabla ya kuanza

  • Tumia anwani ya email ambayo mwaliko ulitumwa kwayo.
  • Unahitaji kuwa na email iliyothibitishwa kwenye akaunti yako ya Keynate.

Hatua

  1. Fungua email kisha ubofye kiungo husika. Kitafungua ukurasa unaoonyesha aliyekualika, jukumu lako na tovuti husika.
  2. Ikiwa hujaingia, bofya Ingia, au Fungua akaunti. Email yako itajazwa kiotomatiki.
  3. Thibitisha email yako ikiwa Keynate itakuomba kufanya hivyo.
  4. Bofya ili kukubali. Unaweza pia kukataa.
  5. Fungua Tovuti zangu. Tovuti zilizoshirikiwa zitaonekana chini ya Zilizoshirikiwa nawe.

Muhimu kujua

  • Kufungua akaunti kupitia mwaliko hakuhitaji malipo yoyote.
  • Jukumu lako ndilo linaloamua kile unachoweza kufanya. Ikiwa jambo fulani limezuiwa, ukurasa utakueleza umwombe mmiliki akubadilishie jukumu.
  • Ili kufungua sehemu ya usimamizi wa tovuti unahitaji kuwezesha uthibitishaji wa hatua mbili kwenye akaunti yako mwenyewe. Uthibitishaji wa hatua mbili
  • Unaweza kujiondoa kwenye timu baadaye kupitia akaunti yako.

Matatizo ya kawaida

"Mwaliko huu umefutwa na mmiliki." Sababu: Mmiliki ameufuta mwaliko huo. Suluhisho: Mwombe mmiliki akutumie mwaliko mpya.

"Mwaliko mpya zaidi umetumwa. Tafadhali tumia kiungo kilicho kwenye email ya hivi punde." Sababu: Mmiliki ametuma tena mwaliko huo upya. Suluhisho: Tumia kiungo kilicho kwenye email ya hivi punde zaidi.

"Mwaliko huu tayari umeshatumika." Sababu: Ulishakubaliwa hapo awali. Suluhisho: Ingia kwenye akaunti kisha ufungue Tovuti zangu.

Mwaliko umekwisha muda wake. Sababu: Kiungo kinafanya kazi kwa siku 7 pekee. Suluhisho: Mwombe mmiliki akutumia mwaliko mpya.

Umeingia kwa kutumia email tofauti. Sababu: Mwaliko huo ulitolewa kwa anwani nyingine ya email. Suluhisho: Toka kwenye akaunti, kisha uingie ukitumia email iliyoalikwa.

Maswali

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, ninahitaji kununua kifurushi?

Hapana.

Zinazohusiana

Maoni

Je, hii imekusaidia?

Inapatikana pia katika

Bado unahitaji usaidizi?